Vitu vyote vilipokwisha kupangwa namna hii, makuhani wal iingia mara kwa mara katika kile chumba cha kwanza kutoa huduma yao ya ibada. Lakini ni kuhani mkuu peke yake ambaye aliruhu siwa kuingia katika chumba cha ndani mara moja tu kwa mwaka. Tena ilibidi aingie huko na damu ambayo aliitoa kwa ajili yake mwe nyewe na kwa ajili ya dhambi za watu walizotenda pasipo kujua. Kwa njia hii, Roho Mtakatifu alikuwa akionyesha kwamba maadamu hema ya kwanza ilikuwa bado imesimama, njia ya kuingia katika Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa bado haijafunguliwa.

Read full chapter